Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LANDESA yaelezea ni vipi ushiriki wao CSW68 unaleta nuru kwa wanawake Tanzania

LANDESA yaelezea ni vipi ushiriki wao CSW68 unaleta nuru kwa wanawake Tanzania

Pakua

Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu yale wanayofanya kutekeleza maudhui ya kipaumbele ya mwaka huu ya kumwezesha mwanamke na mtoto wa kike ili hatimaye kupunguza umaskini na kuimarisha usawa wa kijinsia. Shirika la kiraia la kutetea haki ya ardhi kwa wanawake, LENDESA tawi la Tanzania linaloungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake ni miongoni mwa washiriki  ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Khadija Mrisho, anayeongoza kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke au Stand For Her Land. Khadija anaanza na kile kilichowaleta.

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
5'18"
Photo Credit
Credit: UN News/Assumpta Massoi