Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 JANUARY 2024

13 JANUARY 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza na afya ya watoto chini ya umri wa miaka 5. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?

  1. Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani kote.
  2. Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. 
  3. Makala inatupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP).
  4. Katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kusikia ujumbe wa mlinda amani mwanamke.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'42"