Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahunna Eziakonwa: Nimekuja kuona UNDP inavyoweza kuunga mkono maendeleo ya Burundi

Ahunna Eziakonwa: Nimekuja kuona UNDP inavyoweza kuunga mkono maendeleo ya Burundi

Pakua

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa yuko ziarani nchini Burundi ambako amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii na hata kufika mpaka wa Burundi na DRC kuona uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo. Pia Bi. Eziakonwa amekutana na Rais Evariste Ndaishimye.

“Kwanza kabisa nimemshukuru Rais na nchi kwa kunikaribisha vema katika ziara yangu hii ya kwanza nchini Burundi. Rais na mimi tumejadili mchango wa UNDP katika kuunga mkono maono aliyonayo kwa ajili ya nchi hii. Tunaelewa kwamba kuna maono ya nchi kuwa imechomoza kufikia mwaka 2040 na kuwa imeendelea kufikia 2060. Kama mnavyofahamu UNDP ni shirika la maendeleo na tunataka kuona kile tunachoweza kufanya kuuunga mkono maono haya. Na nimekuja hapa pia kutathimini uimara wa UNDP katika kuisaidia Burundi kwenda katika mwelekeo huu wa maendeleo.”

Bi. Eziakonwa anaendelea kueleza waliyoyazungumza na Rais Ndaishimiye akisema,

“Pia tumejadili kuhusu vijana. Na nimempongeza Rais kama kinara wa mkutano wa vijana wa Afrika kwa ajili ya amani na usalama ambao ulisababisha kupitisha uamuzi wa Muungano wa Afrika kuhusu mchango wa vijana katika kukuza amani na usalama. Tumezungumza kuhusu vijana kwa ujumla na jinsi ya kuwapa fursa vijana kutumia uwezo wao.”

Ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa akiwa ziarani nchini Burundi. Shukrani kwa washirika wetu Mashariki TV ya mjini Bujumbura kwa kufanikisha kutufikishia sauti hii. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
1'47"
Photo Credit
© UNICEF/Karel Prinsloo