Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiweka bidii na kuzingatia mwongozo hakuna linaloshindikana: Mary Keitany 

Ukiweka bidii na kuzingatia mwongozo hakuna linaloshindikana: Mary Keitany 

Pakua

Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya ivi karibuni yalizindua kampeni ya kuhimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora.   Kampeni hiyo maalum ilifanyika jijini Nairobi kwa kuwaalika wanaridha kadhaa wa Kenya wa zamani na wa sasa kwenye ofisi za Umoja wa mataifa. Lengo lilikuwa ni kuzungumza na wanariadha hao kuhusu uhusiano uliopo baina ya mazingira na afya bora ili wawe mabalozi wa kuchagiza hilo katika tasnia yao ambayo mara nyingi hufanyika katika maeneo ya wazi na hewa safi ni muhimu.   Miongoni wa wanariadha hao ni Mary Jepkosgei Keitany anayeshikilia rekodi kadhaa za mbio ndefu au marathoni. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS akianza kwa kutoa historia fupi ya safari yake ya riadha.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Stella Vuzo
Audio Duration
3'56"
Photo Credit
UNEP/Duncan Moore