Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 JANUARI 2024

03 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo kwenye jarida la Habari za Umoja wa Mataifa tunamulika tetemeko la ardhi nchini Japan; Matumizi ya gesi aina ya Naitrojeni Hypoxia kuua mfungwa; Makala ni jinsi sarakasi ilivyomwezesha kijana mkimbizi kupata unafuu wa malipo na mashinani tunakwenda Afar nchini Ethiopia.

  1. Harakati zikiendelea za kunasua watu waliokwama kwenye vifusi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo la kati mwa Japan Jumatatu alasiri kwa saa za huko na kusababisha vifo vya watu 62, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richa. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
  2. Wataalamu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Alice Jill Edwards, anayeshughulikia masuala yanayohusu mateso, na Adhabu nyingine za Kikatili, za kinyume cha utu au za Kushusha hadhi, leo Januari 3 mjini Geneva-Uswisi wameelezea wasiwasi wao kuhusu kukaribia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa kutumia gesi ya nitrojeni hypoxia dhidi ya Kenneth Eugene Smith hapa nchini Marekani. Mwenzangu Anold Kayanda amekifuatilia kisa hicho kwa kina
  3. Makala: John Kibego, mwandishi wa redio washirika Kazi Njema FM huko Hoima nchini Uganda anazungumza na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye kipaji chake cha kucheza sarakasi kimwezesha kupata elimu bora. 
  4. Mashinani: Mama Fatuma, kutoka eneo la Afar, nchini Ethiopia ambaye mwanaye Fatuma ni mnufaika wa huduma za afya ya msingi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF, kwa jamii za wafugaji kuipitia kliniki tembezi ambayo inahakikisha kumfikia kila mama na kila mtoto popote alipo.

 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Sauti
9'58"