Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Tanzania Benki ya Dunia yasaidia ukuzaji wa rasilimali watu na maendeleo

Nchini Tanzania Benki ya Dunia yasaidia ukuzaji wa rasilimali watu na maendeleo

Pakua

Tarehe 19 Desemba mwaka 2019, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 74/245, ambalo liliteua tarehe 4 Desemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Benki kwa kutambua mchango mkubwa wa benki za maendeleo za kimataifa na benki nyingine za maendeleo za kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu na kuchangia uboreshaji wa hali za maisha za wananchi. 

Afrika ni Bara lenye idadi kubwa ya watoto na vijana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatafsiri maana ya takwimu hizo. “Habari hii ni nzuri na vile vile ni mbaya kwetu, Hali hii inaweza kuwa nzuri na yenye tija iwapo tutawekeza kwenye rasilimali watu kwa kuhakikisha uwepo wa afya bora, elimu bora yenye stadi za maisha.”  

Benki ya Dunia, kama moja ya wadau wa Maendeleo katika nchi ya Tanzania kupitia chama chake cha maendeleo cha kimataifa IDA ikaitikia wito huo wa Rais Samia kwa kuwekeza katika nyanja mbalimbali na wanufaika wa miradi hiyo wanaeleza matunda ya uwekezaji.

Dorice Msafiri wa jijini Dar es Salaam ni mnufaika wa miradi ya kuwainua wanawake “Naweza nikawashauri wanawake wengine ambao wangetamani kujiunga na na kozi za uhandisi ni mambo magumu lakini tunaweza wote. Kama ambavyo wanaweza wanaume na sisi pia tunaweza.”

Mradi wau meme vijijini, Sofia Mkuya ni fundi cherehani kutoka Bahi mkoani Dodoma “Tangu umeme ulivyokuja ( katika eneo letu) ninashona mpaka usiku na ninatumia pasi ya umeme kunyoosha nguo situmii mkaa tena.” 

Mradi wa maji vijijini, Herman Mwendowasa mkazi wa kijiji cha Mtisi Villa mkoani Katavi, “Tumeondokana na changamoto ya maji machafu yenye tope maradhi, shida nyingi.” 

Na huko visiwani Zanzibar Benki ya Dunia inaendesha miradi mbalimbali ikiwemo wa nishati ya umeme wa Solar ambao utakapo kamilika unatarajiwa kutoa umeme Kilowati 132 kutoka Kilowati 32 zinazo zalisha hivi sasa. 

Mbali na mchango wao muhimu katika maendeleo ya Tanzania Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Nathan Belete anatoa pongezi, “Tunaipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu kwenye mkakati wao wa ukuaji kwakuzingatia idadi ya watu inaendelea kuongezeka nchini Tanzania hili ni suala muhimu kabisa.”

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
2'5"
Photo Credit
World Bank/ Simone D. McCourte