Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

1 DESEMBA 2022

1 DESEMBA 2022

Pakua

Leo ni Siku ya Ukimwi duniani na jarida linakuletea mada kwa kina tukijikita kabisa nchini Nigeria, moja ya nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ambako ripoti inasema hali si shwari ya maambukizi.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani  

  1. Ikiwa leo ni Siku ya UKIMWI Duniani, Grace Amodu kutoka Nigeria ambaye ni mchechemuzi wa Chama cha kimataifa cha wanawake wanaoishi na virusi vya Ukimwi, ICW, na  Mfamasia wa kijamii nchini Nigeria, anasema anaishi na virusi vya Ukimwi, VVU. Alifahamu kuhusu hali yake ya kuwa na maambukizi ya VVU tangu akiwa na umri wa miaka 7 na tangu wakati huo amekuwa anakunywa dawa. 
  2. Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola bilioni 51.5 kwa ajili ya kusaidia watu milioni 230 mwakani 2023 watu ambao wameelezwa kuwa ukingoni kwani wana uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu.
  3. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa ajili ya siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe Mosi Desemba, amesema ili kuumaliza ugonjwa huo lazima kwanza kukomesha ukosefu wa usawa ambao unakwaza hatua za kusonga mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu unaohatarisha maisha ya watu ulimwenguni kote.
  4. Kupungua kwa maendeleo yaliyopatikana katika muongo mmoja uliopita dhidi ya vifo vya uzazi na watoto wachanga kunatabiriwa barani Afrika, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO iliyotolewa leo
  5. Na hii leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunamulika misemo ya kiswahili na matumizi yake katika lugha hiyo, na mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhadhiri Mwandamizi katika Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anatoa ufafanuzi wa matumizi ya misemo, faida yake na bila kusahau anatoa mifano.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
13'4"