Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaume Morogoro nchini Tanzania wasaidia kufanikisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama

Wanaume Morogoro nchini Tanzania wasaidia kufanikisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama

Pakua

Wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto ambayo ilianza tarehe mosi ya mwezi huu wa Agosti na kuadhimishwa duniani kote kwa jamii kuelimishwa kuhusu umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto imehitimishwa jana tarehe 7. Huko mkoani Morogoro nchini Tanzania, kwa wiki nzima mashirika mbalimbali kwa kushirikiana na serikali yamekuwa yakizungumza na wanajamii ili kufahamu uelewa wao kuhusu suala hili la unyonyeshaji na pia kuwapa elimu panapohitajika. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya Mkoani Morogoro, amehudhuria sherehe za ufungaji wa maadhmisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kata ya Mkambalani Kijiji cha Mkambalani Manispaa ya Morogoro na hii ni taarifa yake.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Hamad Rashid
Audio Duration
1'56"
Photo Credit
© UNICEF/NYHQ2013-1031/Marinovi