Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulikuwa tunawapiga wake zetu lakini elimu imetubadilisha - Wanaume Dodoma.

Tulikuwa tunawapiga wake zetu lakini elimu imetubadilisha - Wanaume Dodoma.

Pakua

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa kwa ushirikiano na wadau, imeonesha kuwa mwanamke 1 kati ya 3 sawa na wanawake milioni 736 wanakumbwa na unyanyasaji kama vile vipigo na ukatili wa kingono kutoka kwa wapenzi wao au wanaume wasio wapenzi wao na idadi ya matukio imeonekana kuwa ya kiwango cha juu katika muongo uliopita. Kwa hivyo, Umoja wa Mataifa umeendelea kuhamasisha jamii kote ulimwenguni kuondokana na unyanyasaji wa namna hiyo na aina nyingine zozote za unyanyasaji. Katika hali inayoonekana kuunga mkono wito wa Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania, Shirika lisilo la kiserikali la COUNSENUTH kupitia mradi wa 'Lishe Kijinsia' limefanikiwa kuzibadili tabia za baadhi ya wanaume ambao walikuwa wanaukumbatia unyanyasaji wa kijinsia. John Kabambala wa redio washirika Kidstime FM ya Morogogoro amefunga safari hadi wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na kutuandalia makala ifuatayo.

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kabambala
Audio Duration
4'4"
Photo Credit
UN Women