Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari ya viuavijidudu kwenye mbogamboga yamulikwa Uganda 

Hatari ya viuavijidudu kwenye mbogamboga yamulikwa Uganda 

Pakua

Ni wazi kuwa mbogamboga ni muhimu katika kuongeza damu na kinga dhidi ya magonjwa mwilini, lakini Je, wafahamu kwamba mbinu za kisasa za kilimo zaweza kugeuza virutubisho kuwa sumu? Na je, unajua kwamba unaweza kutumbukia kwenye magonjwa hatari na kupoteza maisha usipokuwa makini? Basi sikiliza makala hii iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amezungumza na mtaalamu wa lishe kwenye hospitali ya rufaa ya Hoima, Bwana Gilbert Mugabi Makala hii ni mfululizo wa makala zetu za kumulika mwaka wa kimataifa wa mboga mboga na matunda mwaka huu wa 2021 uliotangazwa na Umoja wa Mataifa. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
3'22"
Photo Credit
UN/ John Kibego