Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano kati ya biashara yetu na mazingira ni wa ajabu sana-Wauza miche ya miti Tanzania

Uhusiano kati ya biashara yetu na mazingira ni wa ajabu sana-Wauza miche ya miti Tanzania

Pakua

Biashara ya uuzaji wa miche ya miti nchini Tanzania hususani katika jiji la Dar es Salaam ni ya miaka mingi. Wauzaji wanasema ingawa uhusiano kati ya miti na mazingira ni  wa wazi mno, lakini kwao uhusiano huu ni wa ajabu. Wauza miti wanasema wanauza miti ili iende kuyatunza mazingira, na mazingira kwa haraka yanawalipa kwa kuwaletea mvua ambayo ni muhimu sana kwa biashara yao. Ungana na Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam aliyefunga safari hadi katika eneo la Mabibo, Ubungo Dar es Salaam kukutana na wafanyabiashara hawa. 

Audio Duration
3'30"
Photo Credit
FAO/Rudolf Hahn