Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Roboti janja zatumika Rwanda kukabili COVID-19

Roboti janja zatumika Rwanda kukabili COVID-19

Pakua

Mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, mapema mwaka huu umeibua changamoto kubwa kwa dunia kutokana na virusi hivyo kuathiri mamilioni ya watu ikiwemo barani Afrika. Mathalani nchini Rwanda hadi Julai 7 mwaka huu wa 2020, kumethibitishwa wagonjwa 1,113 na kati yao hao watatu tu wamefariki dunia na serikali imeazimia kuendelea kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.

Soundcloud

Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo UNDP, nchini Rwanda, ukaona ni fursa ya kuibuka na mikakati isiyo ya kawaida ya kupambana na virusi hivyo. UNDP Rwanda ilishirikiana na Wizara ya TEHAMA nchini humo na kufanikisha kuingizwa kwa roboti 5 za kisasa ambazo zimeonesha makali yake huko China, Korea Kusini na Uholanzi katika kupambana na virusi vya Corona. Je ni kwa vipi? Ungana basin a Hilda Phoya katika makala hii.

 

Audio Credit
Loise Wairimu/Hilda Phoya
Audio Duration
3'52"
Photo Credit
UN RWANDA