Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO msituchoke, endeleeni kutuimarisha - Wanakikundi Umoja ni Nguvu Kakonko

FAO msituchoke, endeleeni kutuimarisha - Wanakikundi Umoja ni Nguvu Kakonko

Pakua

Wanawake wakulima wa kikundi cha Umoja ni Nguvu katika kata ya Katanga, wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma wameshindwa kuficha furaha yao kutokana na mafunzo ya kilimo bora kinachohimili mazingira. Sasa mavuno ni ya kutosha, mashamba yao  yalistawi na kilimo chao siyo tu kimeleta manufaa kwenye mlo bali pia hata kusaidia watoto wao. Je ni kwa vipi? Assumpta Massoi aliwakuta wanawake hao wakiwa shambani asubuhi wakifanya palizi huku wakiimba na alizungumza na mwezeshaji wao Paskazia Kazibwa ambaye katika sehemu hii ya pili anaelekeza shukrani zao kwa FAO ambayo imewawezesha kupitia mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa mkoa wa Kigoma au Kigoma Joint Programme. 

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
3'20"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi