Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 116 kuzaliwa miezi 9 baada ya COVID-19 kutangazwa janga, je changamoto ni zipi?

Watoto milioni 116 kuzaliwa miezi 9 baada ya COVID-19 kutangazwa janga, je changamoto ni zipi?

Pakua

Kuelekea siku ya mama duniani tarehe 10 mwezi huu wa Oktoba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linakadiria kuwa watoto milioni 116 watakuwa wamezaliwa wiki 40 tangu ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 utangazwe kuwa janga la kimataifa tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sauti ya mama mjamzito katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya serikali mjini Zomba nchini Malawi, akijifungua, akiwa amezingirwa na wakunga na madaktari katika mazingira yaliyozoelea ambayo sasa na COVID-19 yamebadilika.

UNICEF katika taarifa yake iliyotolewa leo jijini New York, Marekani inasema kuwa, wanawake wanaojifungua katika kipindi cha sasa na watoto wao wanakumbana na machungu mapya ikiwemo hatua za kuzuia kuchangamana, ukosefu wa vifaa vya matibabu, na amri za kutotembea hovyo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore amenukuliwa akisema kuwa mamilioni ya wazazi duniani kote wanaanza safari ya uzazi wakihofia kwenda vituo vya afya kwa hofu ya maambukizi  na kutokana na amri ya kutotembea hovyo.

 Amesema ni vigumu sana kufikiria ni kwa jinsi gani gonjwa la Corona limeathiri uzazi na hivyo UNICEF inaonya kuwa, hatua za kuzuia watu kutoka majumbani mwao zinaweza kuvuruga huduma za afya za kuokoa maisha kama vile huduma za kujifungua.

UNICEF inaonya kuwa ingawa ushahidi unaonesha kuwa wajawazito hawaathiriwi zaidi na COVID-19 kama ilivyo kwa watu wengine, serikali zinapaswa kuhakikisha kuwa bado wanapata huduma za kabla, wakati na baada ya kujifungua.

Ijapokuwa bado haijafahamika iwapo virusi vya Corona vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujautizo, UNICEF inasihi wajawazito wachukue hatu kujikinga na kufuatilia dalili za virusi hivyo.

Audio Duration
1'52"
Photo Credit
UNICEF/Ilvy Njiokiktjien