Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Mwanza Tanzania wabuni mashine ya kusambaza maji kiteknolojia

Vijana Mwanza Tanzania wabuni mashine ya kusambaza maji kiteknolojia

Pakua

Vijana jijini Mwanza Tanzania wamebuni mradi wa maji safi na salama kwa kutengeneza mashine za kielekroniki ikiwa ni sehemu ya juhudi zao kutimiza lengo namba sita la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDG ambayo yanategemewa kuwa yamekamilishwa kikamilifu ifikapo mwaka 2030. Lengo namba 6 la SDGs linazungumzia upatikanaji wa maji safi na salama na kujisafi. Vijana hao wahitimu wa Chuo Kikuu wameupa jina la ECO WATER mradi wao huo na mtumiaji hutumia kadi maalumu ya kielektroniki ili kupata huduma ya maji.  Maelezo zaidi yako katika makala hii ambayo imeandaliwa na Evarist Mapesa na Nyota Simba  na kusimuliwa na Nyota John Simba kutoka Redio washirika Redio SAUT FM ya jijini Mwanza.

 

Audio Credit
Loise Wairimu/ Nyota John Simba
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
© UN-Habitat/Kirsten Milhahn