Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulinde udongo la sivyo tutakosa chakula- FAO

Tulinde udongo la sivyo tutakosa chakula- FAO

Pakua

Hii leo ikiwa ni siku ya udongo duniani, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo duniani, FAO linataka hatua zaidi kuepusha mmomonyoko wa udongo kwa ajili ya mustakabali bora. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Mkurugenzi wa FAO anayehusika na masuala ya ardhi na kampeni ya siku ya leo, Eduardo Mansur, amesema udongo ambao unahifadhi robo ya bayonuai na kuchangia asilimia 95 ya chakula, hivi sasa unakabiliwa na hatari kubwa.

Amesema ingawa mmomonyoko wa udongo unatokea katika maeneo yote, lakini kwa kiasi kikubwa unaweza kuchochewa kwa mara maelfu kutokana na kilimo kisichotumia mbinu endelevu na pia matumizi haramu ya ardhi ikiwemo ukataji miti kiholela hali inayoharibu afya ya udongo kwa ajili ya kilimo chenye tija.

Kama hiyo haitoshi amesema kuwa iwapo kasi ya sasa itaendelea, mmomonyoko wa udongo unaweza kupunguza kiwango cha uzalishaji wa mazao kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2050 na kwamba…

“Unahitaji miaka 1,000 kupata sentimeta 1 ya tabaka la juu la udongo, lakini sentimeta hii moja ya udongo inaweza kupotezwa na mvua kubwa.”

Kwa mantiki hiyo amesema ili kulinda udongo…

(Sauti  ya Eduardo Mansur)

“Wakulima na watumiaji wengine wa ardhi wanaweza kuanza kutumia mbinu bora za matumizi ya udongo katika mazingira ambayo yanaruhusu. FAO kwa upande wetu tuko tayari kuwasaidia.”

FAO: Siku za UN, Udongo, WSD19

 

 

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'18"
Photo Credit
FAO/Marco Longari