Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimejitolea kukomesha ajira kwa watoto Uganda sababu nimeipitia asema Namirembe

Nimejitolea kukomesha ajira kwa watoto Uganda sababu nimeipitia asema Namirembe

Pakua

Wahenga walisema siri ya mtungi aijuaye kata na uchungu wa ajira ya mtoto anaujua mtoto aliyeipitia, kauli hiyo imetolewa na Molly Namirembe mwanaharakati wa kupambana na ajira ya watoto nchini Uganda ambaye yeye mwenyewe alipitia madhila hayo na jinamizi lake linamtesa hadi sasa. Kupitia mradi wa SCREAM unaosaidiwa na shirika la kazi duniani ILO Namirembe amedhamiria kupambana na ajira hiyo nchini mwake. 

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'43"
Photo Credit
ILO/Marcel Crozet