Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ni sehemu ya maendeleo na bila mwalimu hakuna elimu-Mwalimu Tabichi

Elimu ni sehemu ya maendeleo na bila mwalimu hakuna elimu-Mwalimu Tabichi

Pakua

Leo katika mada kwa kina tunaangazia siku ya walimu duniani ambayo huadhimishwa Oktoba 5 kila mwaka, mwaka huu kaulimbiu ikiwa ni “walimu vijana, mustakbali wa tasnia hii.” Lengo la siku ya walimu ikiwa ni kuwaenzi walimu kote ulimwenguni, kupongeza mafanikio na kuangalia changamoto zilizopo  kwa ajili ya kuimarisha tasnia hiyo. Mgeni wa siku ya leo kwa sasa anashikilia tuzo ya mwalimu bora kimataifa, tuzo ambayo ametunukiwa mapema mwaka huu kufuatia kujitolea kwake katika kazi ualimu. Mwalimu Peter Tabichi kutoka Kenya ambaye ni mwalimu wa somo la hisibati na fizikia katika shule ya sekondari ya Keriko iliyoko kaunti ya Nakuru nchini Kenya amezungumza na Grace Kaneiya wiki chache zilizopita hapa jijini New York Marekani kuhusu ushindi alioupata na matarajio yake  katika siku zijazo.

 

Audio Credit
Peter Tabichi
Sauti
5'57"
Photo Credit
UN News/Grece Kaneiya