Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akili Bandia yaanza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya nchini Tanzania

Akili Bandia yaanza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya nchini Tanzania

Pakua

Mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu akili bandia, au AI ukiendelea huko Geneva, Uswisi, nchini Tanzania inaelezwa kuwa tayari akili bandia imeanza kutumika kuboresha huduma za afya hasa katika maeneo yenye uhaba wa daktari.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Castory Munishi, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba, Muhimbili, MUHAS nchini Tanzania, chuo ambacho hivi karibuni kiliendesha mdahalo kuhusu akili bandia na nafasi yake katika kuimarisha huduma za afya.

Akihojiwa kwa njia kutoka Dar es salaam Tanzania na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa, Munishi ametolea mfano daktari msaidizi, Daktari Elsa.

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'4"
Photo Credit
ITU/D. Procofieff