Msichana si kitega uchumi Samburu tafuteni biashara nyingine:Lerosion

28 Mei 2019

Ndoa za utotoni bado ni mtihani mkubwa katika jamii ya Wasamburu nchi Kenya ambazo mizizi yake ni ya toka enzi za mababu. Na zimedumu kwa muda mrefu kwa sababu zinachukuliwa kama ni chanzo cha utajiri kwa wazazi hasa kina baba.

Lakini hivi sasa wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii, kidini na hata serikali wamelivalia njuga kwa kuelimisha athari zake kwa mustakabali wa msichana  hususan wa kupata elimu. Miongoni mwa wanaharakati whao ni Emily Rosa Lerosion mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la New Dawn Pacetter ambalo dhamira yake kuu ni kumkwamua msichana wa Kisamburu.

Katika makala hii Flora Nducha amemuuliza tatizo  la watoto wa Kike kutosoma katika jamii ya Samburu ni kubwa kiasi gani?

 

Audio Credit:
Patrick Newman/ Flora Nducha/ Emily Lerosion
Audio Duration:
4'34"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud