Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji wa nyuki na mafundi seremala Kigoma wapewa mafunzo ili kuboresha mizinga na uzalishaji bora wa asali.

Wafugaji wa nyuki na mafundi seremala Kigoma wapewa mafunzo ili kuboresha mizinga na uzalishaji bora wa asali.

Pakua

Tarehe 20 ya mwezi huu wa Mei ilikuwa ni siku ya nyuki duniani msisitizo ukiwa katika kutunza wadudu hao wachavushaji wa maua ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa chakula. Makala yetu kwa kina inaangazia ni kwa vipi wafugaji wa nyuki wanaweza kutunza mazingira na wakati huo huo kujipatia kipato kwa njia fanisi zaidi. Hivyo basi tunamulika mradi wa pamoja wa Kigoma unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa  Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo FAO. Hivi karibuni liliendesha mafunzo kwa wafugaji wa nyuki na mafundi seremala ili kuboresha mizinga na uzalishaji wa asali bora. Je nini kilifanyika? Ungana basi na Grace Kaneiya

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Audio Duration
5'31"
Photo Credit
FAO