Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo na majeruhi Yemen inatisha:UNHCR

Idadi ya vifo na majeruhi Yemen inatisha:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na lina hofu kubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na majeruhi wakati mashambulizi yalipoughubika mji wa Sana’a nchini Yemen jana Alhamisi

Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamelaani mashambulizi ya anga yaliyofanyika jana Alhamisi kwenye mji mkuu wa Yemen, Sana'a na kusababisha vifo na majeruha.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Jens Laerke amenukuu ripoti za awali zisemazo kuwa watoto watano wameuwawa na watu wengine 16 wamejeruhiwa wakiwemo wahudumu wa afya.

Bwana Laerke ameongeza kwamba,“Majeruhi akiwemo watoto walipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu, kuna baadhi ya hospitali ambazo zinaendelea na shughuli zake, mbili zikiendeshwa kwa hisani ya wadau wa misaada ya kibinadamu na wamepokea majeruhi.”

Amesema taarifa kamili kuhusu shambulio hilo hazijulikani na kwamba, hana uhakika kuhusu eneo kamili ambako shambulio lilitokea na kwamba mitaa tofauti ililengwa mjini Sana’a.”

Wakimbizi pia ni waathirka wa vita 

Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na lina hofu kubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na majeruhi kufuatia shambulio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic amesema wakimbizi ni miongoni mwa majeruhi na waathirika ambapo mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Somalia na binti yake ni miongoni mwa majeruhi wanaopatiwa matibabu ya wagonjwa mahtuti hospitalini.

Amesema kuwa matukio kama hayo ambayo yanasababisha maisha ya raia kupotea na majeruhi yanaendelea kuonyesha ukweli kwamba vita nchini Yemen vitawabebesha gharama kubwa raia na kwamba raia ni lazima walindwe na pande zote katika mzozo lazima zihakikishe kwamba zinazingatia wajibu wao chini ya sheria za kibinadamu za kimataifa.

Kuna zaidi ya wakimbizi na waoomba hifadhi 275,000 nchini Yemen wengi wao ambao ni zaidi ya asilimia 90 wanatoka nchini Somalia. Hali ya wakimbizi, waomba hifadhi na wahamiaji nchini Yemen ambayo tayari ilikuwa mbaya sasa imezorota zaidi kutokana na vita vinavyoendelea.

UNHCR inasema tangu mwaka 2017 ilianzisha mradi wa kuwarejesha nyumbani kwa hiyari wakimbizi na waomba hifadhi ambao shirika hilo linaufanya kwa ushirikiano na wadau wengine likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji , IOM na miongoni mwa msaada wanaowapatia watu hao ni nyaraka muhimu, usafiri na fedha wakiwa Yemen ili ziwasaidie safarini , lakini pia msaada wa kuwarejesha na kuwajumuisha kwenye jamii pindi wanapowasili Somalia.

UNHCR inasema Jumatatu wiki hii wakimbizi 105 waliondoka bandari ya Aden kuelekea bandari ya Berbera Somalia kama sehemu ya mpango wa kurejea nyumbani kwa hiyari na hivyo kufanya jumla ya wakimbizi ambao wamerejea nyumbani kupitia mpango huo kufikia 4068.

Ghasia zinatishia usambazaji wa chakula

Shirika la Chakula Ulimwenguini WFP linasema linafuatilia kwa karibu hali kote nchini Yemen

Limesema ghasia ambazo zimeibuka hivi karibu katika maeneo ya Hodeidah, Sana’a na Dhalea zinatia wasi wasi sana.

Msemaji wa WFP Herve Verhoosel, alisema WFP inajitahidi kupunguza athari zinazotokana na ghasia katika oparesheni zao zinaweza kuwafikia wale wanaohitaji misaada

WFP kwa mara nyingine inatoa wito wa kutokwepo vizuyizi katika kuyafikia maeneo mengine ya nchi.

Hii ni muhimu ikiwa tunataka kufikia lengo letu la kuwapa chakula watu milioni 12 nchini Yemen, ambao hata hawajui chakula chao kitatoka wapi. Hatua za WFP hadi sasa zimezuia halia mbaya ya njaa nchini Yemen. Tunahitaji kuendlea kutoa misaada yetu, ilisema taarifa ya Herve Verhoosel.

Ilisema kundi la kiufundi huku Red Sea Mills, Hodeidah linapiga hatua nzuri. Ukarabati kwenye maghala na pia mashine za kisaga unakaribia kukamilika na kwa wakati wowote ngano itaanza kuwekwa dawa.

Ikiwa oparesheni zetu zitaendelea bila tatizo, tuna matumaini kuwa hivi karibuni tutaanza kusaga mgano kisha taunze kusafirisha kwa watu wanaoihitaji sana, ilisema taarifa hiyo ya WFP.

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na lina hofu kubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na majeruhi wakati mashambulizi yalipoughubika mji wa Sana’a nchini Yemen jana Alhamisi

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
1'47"
Photo Credit
OCHA/Charlotte Cans