Mipango miji ni hatua ya kwanza katika ujenzi wa miji salama
Lengo namba 9 la malengo ya maendeleo ya endelevu ya Umoja wa Mataifa yanayofikia ukomo 2030, linazungumzia miundombinu yenye mnepo, kuwekeza katika sekta
ya viwanda endevelu, na kukuza ubunifu. katika sekta hiyo Umoja wa Mataifa unazihimiza serikali na asasi mbalimbali za kiraia kuzingatia ubora wa miundombinu ili kujenga miji iliyo salama na yenye ustawi bora katika jamii.
Wito huo umeanza kuitikiwa na serikali mbalimbali, mathalani nchini Uganda , serikali ya manispa ya Hoima imechukuwa jukumu la kuhakilisha ujenzi wa barabara na miundombinu vinakidhi viwango stahiki kwa manufaa ya taifa na watu wake. Mwandishi wetu nchini humo John kibego amezungumza na meya wa Hoima ambaye ameweka bayana mikakati madhubuti ya ujenzi wa mji huo kwa kuzingatia taratibu za mipango miji.
Kwa undani zaidi kuhusu hilo ungana naye.