Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kuhifadhi matumbawe zazaa matunda

Harakati za kuhifadhi matumbawe zazaa matunda

Pakua

Matumbawe, hupatikana kwenye zaidi ya nchi 100 duniani kote ikiwemo nchi za visiwa vidogo, SIDS na mataifa mengine yanayoaendelea. Licha ya umuhimu wake katika kusaidia uhai ndani ya bahari, matumbawe yako hatarini kutoweka kutokana na shughuli za binadamu zinazochochea mabadiliko ya tabianchi. Umoja wa Mataifa unasema kuwa theluthi mbili za matumbawe duniani ziko hatarini na ndio maana lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi na matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake kwa ajili ya maendeleo endelevu. Je nini kinafanyika? Leo tunakwenda Kenya moja ya nchi zenye matumbawe kuangazia harakati za kuhifadhi na mwenyeji wako katika makala hii ni Grace Kaneiya.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Grace Kaneiya
Audio Duration
4'23"
Photo Credit
Coral Reef Image Bank/Jayne Jenk