Jamii zilizo jirani na bahari ni wadau wakuu katika kulinda bahari- Soares
Baada ya siku tano za mijadala na maonesho mbalimbali, mkutano wa pili kuhusu baharí umefikia tamati huko Lisbon nchini Ureno ambako Miguel de Serpa Soares ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisheria amesema mwelekeo wa kulinda na kuhifadhi baharí unatia matumaini kwa kuzingatia yaliyokubaliwa, changamoto zilizoko sambamba na fursa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.