Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana mkimbizi aanzisha radio kambini, wakimbizi wakisisitiza umuhimu wake Kyangwali, Uganda

Kijana mkimbizi aanzisha radio kambini, wakimbizi wakisisitiza umuhimu wake Kyangwali, Uganda

Pakua

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya radio hii leo, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limsema radio inahabarisha, kubadilisha maisha na kuwaleta watu pamoja licha ya utofauti wao. Zaidi ya hayo radio ni chombo muhimu katika kukabiliana na ukatilia na kuenea kwa mizozo hususan katika maeneo kunakoshuhudiwa hali hiyo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa radio ni muhimu kwa watu ambao wanajikuta ukimbizini kufuatia uwepo wa ukatili au mizozo wanakotokea. Kwa kuzingatia umuhimu wa radio kijana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC amebuni radio ambayo ni mahsusi kwa ajili ya wakimbizi na jamii inayowazingira kambini Kyangwali nchini Uganda ambaye alipata fursa ya kuzungumza na mwandishi wetu nchini humo John Kibego.

Audio Credit
Flora Nducha/John Kibego
Sauti
4'
Photo Credit
UNESCO