Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya kuwa mhandisi, Nadhifa Zubeir ni mama na mke

Zaidi ya kuwa mhandisi, Nadhifa Zubeir ni mama na mke

Pakua

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, katika masomo ya ngazi ya juu takribani asilimia 30 pekee ya wanafunzi wa kike ndiyo wanachagua masomo yanayohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati. Moja ya sababu zinazotajwa kuchangia hali hiyo ni pamoja na mfumo dume unaowafanya wasichana na wanawake kushughulika zaidi na kazi za kifamilia na hivyo kuwapa nafasi zaidi wanaume kung’ara katika masomo.

Lakini kwa upande wa mhandisi Nadhifa Zubeir Hassan anawashukuru wazazi wake kwani walimuunga mkono akasoma masomo ya sayansi na hivi sasa uungwaji mkono anaoupata kutoka kwa mume wake na familia yao ya watoto wawili kumemfanya kuwa kinara katika kazi yake ya ufundi wa ndege katika shirika la ndege la Tanzania Air Tanzania.

 

Soundcloud
Audio Credit
Arnold Kayanda/Stella Vuzo/ Nadhifa Zubeir
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
Nadhifa Zubeir