Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Bolivia waanza kufuata utaalam wa kijadi kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Wakulima Bolivia waanza kufuata utaalam wa kijadi kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Wakati viongozi wa ndunia wakiendelea kukuna vichwa mjini Katowice nchini Poland kusaka dawa mujarabu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye mkutano wa COP24 hadi Disemba 14, jinamizi hilo limeendelea kuziathiri jamii mbalimbali duniani.  Nchini Bolivia, takriban asilimia 40 ya watu wake wameathirika na mabadiliko ya tabianchi. Ukame  wa kila mara,  mafuriko, na theluji  vinaharibu mimea na kutishia uhakika wa chakula na mustakabali wa watu hao.

Sasa wakulima wameamua kugeukia utalaamu wa kijadi ili kujenga mnepo wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. Kwa undani Zaidi wa nini wanachokifanya ungana na Anold kayanda  kwenye makala hii.

 

 

Audio Credit
Siraj Kalyango/Anold Kayanda
Audio Duration
3'17"
Photo Credit
Ifad/Reproduction