Chonde chonde wabolivia kaeni mbali na machafuko:Guterres
Kufuatia hali ya wasiwasi inayoendelea nchini Bolivia baada ya kujiuzulku kwa rais wa nchini hiyo Evo Morales mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka raia wote wa nchi hiyo kujizuia na machafuko na mamlaka kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia wote, maafisa wa serikali na raia wa kigeni.