Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yashirikisha wavulana vita dhidi ya ukeketaji Tanzania

UNICEF yashirikisha wavulana vita dhidi ya ukeketaji Tanzania

Pakua

Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa unatumia mbinu mbalimbali kufikisha  ujumbe wa kuepusha watoto wa kike dhidi ya ukatili. Vitendo vya ukatili kama vile ukeketaji umekwamisha maendeleo ya mtoto wa kike na zaidi ya yote wapo baadhi ya wanaume wanaoamini kuwa mtoto wa kike asiyekeketwa hafai katika jamii. Ni kwa kuzingatia hilo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania limeibuka na mbinu ya siyo tu mabingwa wa kutetea watoto bali pia kuhusisha vijana wa kiume katika kampeni ya kuhamasisha jamii kulinda watoto wa kike. Je nini kinafanyika? Ungana na Siraj Kalyango katika makala ya fuatayo kwa undani zaidi.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'16"
Photo Credit
Elimu ya kuhamasisha watoto na jamii kuhusu athari za ukeketaji. (Picha:© UNICEF/UNI144402/Asselin)