Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya usalama isiwe kizingiti kwa wasaka hifadhi kutoka Honduras

Hofu ya usalama isiwe kizingiti kwa wasaka hifadhi kutoka Honduras

Pakua

Wakati msafara wa mamia ya raia wa Amerika ya Kati ukiripotiwa kuvuka mpaka na kuingia Mexico mwishoni mwa wiki, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, Felipe Gonzalez, ametoa wito kwa nchi kutoziweka rehani haki za binadamu za wahamiaji hao kwa  sababu ya hofu ya masuala ya usalama. Assumpta Massoi na tarifa kamili.

Katika mahojiano maalumu na UN News, bwana Gonzales amesema msafara huo kutoka Amerika ya Kati ni mfano mmoja tu wa hali inayotokea kila siku katika maeneo mengi duniani na kuzusha mjadala unaoendelea wa mkataba wa kwanza wa kimataifa kuhusu wahamiaji unaotarajiwa mwezi Desemba utakavyosaidia changamoto hii . Kufuatia wimbi hilo la wahamiaji wa Amerika ya Kati amessiitiza kwamba

 “Ni muhimu kufikiria kwamba sio kwa bahati mbaya msafara wa watu wote hawa wanakuja nchini Marekani, hii ni kutokana na hali mbaya wanayokabiliana nayo katika nchi wanakotoka, hivyo natoa wito kwa nchi kutochukua hatua kutokana na hofu ya usalama bali kutilia maanani haki za binadamu.”

Na je mkataba wa kimataifa wa uhamiaji unaosubiriwa kwa hamu mnamo Desemba utaleta ahuweni yoyote katika zahma hii?

“Hicho sio chombo cha haki za binadamu lakini ni sehemu ya haki za binadamu , hivyo nadhani ni hatua muhimu, na nadhani utendaji wa mkataba huo wa kimataifa wa uhamiaji utategemea na aina ya utekelezaji itakayofanyika na utayari wa nchi na Umoja wa Mataifa kusonga mbele katika suala hili.”

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'26"
Photo Credit
UNICEF/Tanya Bindra