Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu ndio muarobaini wa SDGs

Takwimu ndio muarobaini wa SDGs

Pakua

Wataalam wa kimataifa wa takwimu kutoka ofisi za kitaifa, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s, wanazuoni, na mashirika ya kimataifa na kikanda, wamekusanyika mjini Dudai katika Falme za Kiarabu kuanzia leo katka jitihada za kusongesha mbele mchakato wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s.

 

Katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa siku tatu utakaokunja jamvi Jumatano wiki hii, wataalam hao watazindua suluhu bunifu ya kuboresha takwimu za wahamiaji, masuala ya afya, jinsia na maeneo mengine muhimu kwa ajili ya maendeleo endelevu . Akisistiza umuhimu wa takwimu katika utekelezaji wa SDG’s wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema,

“Ili kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu tutahitaji takwimu zaidi na zilizo bora, sahihi, zinazowakilisha na kujumuisha wote , tutaweza kuelewa changamoto zinazotukabili na kuweza kubaini suluhu muafaka kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu.”

Mkutano huo wa pili wa kila mwaka unaambatana na matukio na vikao takribani 80 na unaonekana kuwa ni fursa nzuri kwa wazalishaji na watumiaji wa takiwmu katika kusaka njia bora za kuto takwimu kwa watunga sera  na raia katika nyanja zote za SDG’s.

Naye  Liu Zhenmin, mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa ajili ya masuala kiuchumi na kijamii akiunga mkono hoja hiyo amesema“ Ni muhimu kuwa na tamwimu sahihihi, za kuaminika, kwa wakati na zilizokusanywa pamoja kwa ajili ya kufuatilia masuala ya kiuchumi, kijamii na malengo ya mazingira katika ajenda ya 2030. Katika kongamano la Umoja wa Mataifa la takwimu natarajia kuundwa kwa ushirika mpya, kutangazwa kwa ahadi na kuongezwa kwa msaada.”

Mkutano huo unafanyika miezi miwli kabla ya kupitishwa na nchi wanachama mkataba wa kimataifa wa uhamiaji , ambao utakuwa mkataba wa kwanza kabisa  wa Umoja wa Mataifa duniani ulio na lengo la pamoja kuhusu uhamiaji wa kimataifa.

Miongoni mwa mada kuu zitakazopewa kipaumbele ni ufadhili kwa ajili ya takwimu na kumbukumbu na njia za kuziba pengo la ufadhili na takwimu zilizopo katika nchi nyingi .

Audio Duration
2'21"
Photo Credit
NASA Earth Observatory/Lauren Dauphin