Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa chakula bado changamoto Burundi

Ukosefu wa chakula bado changamoto Burundi

Pakua

Takwimu za mashirika ya Umoja wa Mataifa  nchini Burundi zinasema watu zaidi ya Milioni 3 nchini humo wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu. Watu milioni moja kati ya hao wana tatizo la ukosefu wa chakula. Hali hiyo imefanya watoto wengi kusumbuliwa na maradhi ya utapiamlo. Mashirika kadhaa ya wahisani yameanza kujishughulisha na kuwapa chakula watoto wenye tatizo la utapia mlo.  Kufuatia hali hiyo ,  Burundi inajikuta  katika  wasiwasi  mkubwa  wa kuweza  kutimiza lengo    la maendeleo endelevu la kutokomeza njaa  ifikapo mwaka 2030 . Mwandishi wetu wa maziwa Makuu , Ramadhani KIBUGA ametembelea kituo kimoja kinachotoa chakula kwa watoto ili kupambana na  njaa na utapia mlo.Ungana naye katika makala hii

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango /Ramadhani Kibuga
Sauti
4'7"
Photo Credit
Watoto nchini Burundi wanaopokea mlo shuleni.(Picha:WFP/Didier Bukuru)