Je Tanzania ya kijani inawezekana? Dk Mwakaluka
Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele katika uhifadhi wa mazingira ili kubabiliana na tatizo la tabianchi. Kampeni moja wapo katika ulinzi wa mazingira ni uhifadhi wa misitu ya asili na pia upandaji miti ili kufukia lengo la Umoja wa Mataifa la kuongeza misitu yote ya dunia kwa asilimia 3 ifikapo mwaka 2030.
Tanzania kwa upande wake imejiwekea mikakati ya maendeleo ya kitaifa katika uhifadhi wa misitu ya mwaka 2021 ya kuweza kuongeza ukubwa wa misitu ya asili kupitia kampendi " panda mti" yenye lengo la kupanda miti milioni 100 kila mwaka.
Mwandishi wetu Patrick Newman alipata fursa ya kuzungumza na Dk Ezekiel Mwakaluka ambaye ni mkurugenzi wa Misitu na nyuki katika wizara ya maliasili na utalii nchini tanzania . Je nini alichozungumza kuhusu utekelezaji wa mikakati ya serikali kuhusu uhifadhi ya misitu Tanzania? Ungana naye katika makala hii.