Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pasipo na amani, Tanzania tunakwenda kuleta amani- Balozi Mahiga.

Pasipo na amani, Tanzania tunakwenda kuleta amani- Balozi Mahiga.

Pakua

Tanzania imesema licha ya kupoteza askari wake kwenye operesheni za ulinzi wa amani, bado itaendelea kushiriki kwenye operesheni  hizo kwani inatambua kuwa bila amani hakuna maendeleo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huko Dar es Salaam, Tanzania huku akitanabaisha kuwa pasipo na amani ndio Tanzania inakwenda kuleta amani. Kwa kina zaidi fuatilia ripoti hii ya Assumpta Massoi iliyofanikishwa kutokana na mahojiano  yaliyofanywa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC, Dar es salaam.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'39"
Photo Credit
Askari wa Tanzania walio kwenye kikosi cha MONUSCO cha kujibu mashambulizi, FIB wakiwa sambamba na askari wa jeshi la serikali ya DRC. Hapa ni Beni, jimbo la Kivu Kaskazini. (Picha:MONUSCO Force)