Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huko Gaza wahudumu wa afya wahaha kutibu majeruhi

Huko Gaza wahudumu wa afya wahaha kutibu majeruhi

Pakua

Wahudumu wa afya huko Gaza, Mashariki ya Kati hivi sasa wanahaha kutibu zaidi ya majeruhi 2700 wa ghasia za jana zilizosababisha vifo vya watu 58. Taarifa zaidi an Assumpta Massoi.

 

Taarifa ya Assumpta Massoi

 

Umoja wa Mataifa umesema vituo vya afya vimezidiwa uwezo huku majeruhi wengine wakilazimika kuachwa kwenye veranda za hospitali kwa kuwa idadi ya wagonjwa ni wengi, na vifaa vya matibabu ni vichache.

 

Tarik Jasarevic ni msemaji wa shirika la afya ulimwenguni, Geneva, Uswisi.

 

Sauti ya Tarik Jasarevic

“Uwezo wa huduma za afya Gaza ni mdogo sana na umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa kwa zaidi ya miaka 10 ya migogoro inayoendelea. Wamekuwa na tatizo la ukosefu wa vifaa na dawa. Mwezi huu pekee tumegundua kwamba vituo viwili kati ya vitano havina huduma ya kutosha. Dawa za huduma za dharura kama viuavijasumu zinahitajita .”

 

Nayo ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya umoja huo, OCHA imesema majeruhi 1,300 kati ya 2700 hao walishambuliwa kwa risasi za moto kutoka askari wa Israel.

 

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

 

Sauti ya Jens Laerke

 

“Mpaka hapo hakuna alipoteza maisha upande wa Israel, isipokuwa mwanajeshi mmoja wa aliyejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu. Baadaye tumepata taarifa ya kifo kimoja upande wa Israel.”

 

Naye mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Micheal Lynk amelaani kitendo hicho cha askari wa Israel kushambulia raia akitoa wito  kwa serikali ya Israel isitishe matumizi ya silaha za moto yasiyo ya lazima  kwa waandamanaji wa kipalestina  kwenye ukanda wa Gaza .

Audio Credit
Taarifa ya Assumpta Massoi
Audio Duration
1'37"
Photo Credit
Save the Children/Mohamed N Ali