Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia wafungua milango ya utalii

Somalia wafungua milango ya utalii

Pakua

Nchini Somalia mashambulizi ya Al-Shabaab na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamesababisha maelfu ya raia kupoteza makazi na wengine kukimbilia nchi jirani. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini humo, UNSOM, kwa kushirikiana na serikali unatumia njia mbalimbali kuhakikisha mkataba wa amani umetekelezwa ili  amani irejee nchini humo, ambamo ni moja ya nchi barani Afrika inayoweza kuvutia watalii wengi. 

Na kama ujuavyo amani na usalama ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 16 likitaka amani, haki na taasisi imara.

Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anamulika hali halisi katika sekta ya utalii wa bahari na mazingira nchini humo na jinsi amani na usalama vinavyochagiza ziara za watalii.

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
Pwani ya Kismayo Somalia kwenye bahari ya Hindi. Picha na UM/Stuart Price