Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukimkomboa mwanamke, umeikomboa jamii

Ukimkomboa mwanamke, umeikomboa jamii

Pakua

Nchini Uganda serikali imeamua imechukua hatua ya kuwawezesha wanawake vijijini ili wajiinue kiuchumi lakini pia waache kuwa tegemezi, kwa kuwapa mikopo midogo midogo ambayo inawapa fursa ya kufanyia shughuli za kimaendeleo. Lengo kubwa ni kuhakikisha mwanamke wa kijijini asalii nyuma na kuzama katika lindi la umasikini.

Mwandishi wetu John kibego amewatembelea baadhi ya wanawake hao katika wilaya ya hoima kushuhudia shughili wanazofanya.  Ambatana nao katika Makala hii

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'13"
Photo Credit
UN Photo/Albert Gonzalez Farran