Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani Afrika latiwa saini

Azimio la Kigali kuhusu eneo la biashara huru barani Afrika latiwa saini

Pakua

Zaidi ya marais na naibu marais 19 wa Afrika wameshiriki kwenye utiaji saini wa azimio hilo mjini Kigali, Rwanda baada ya kikao kisicho cha kawaida cha viongozi wa Muungano wa Afrika, AU.

 Akizungumza na Priscilla Lecomte, wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika, ECA mjini humo, Ali Mufuruki ambaye ni Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa kundi la kampuni za Infotech nchini Tanzania, amezungumzia mambo muhimu ya kufanikisha makubaliano hayo.

 (Sauti ya Ali Mufuruki)

 Akaenda mbali zaidi kuzungumzia umuhimu wa nishati katika kufanikisha makubaliano hayo..

 Sauti ya Ali Mufuruki)

 Baadhi ya viongozi wa Afrika wametia saini itifaki ya watu kutembea huru barani humo, itifaki ambayo itawezesha waafrika kupata hati ya kusafiria ya Afrika.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'21"
Photo Credit
ECA