Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM Lebanon akutakana na wakimbizi wa Syria

Mratibu wa UM Lebanon akutakana na wakimbizi wa Syria

Pakua

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Sigrid Kaag ametembelea bonde la Bekaa nchini Lebanon ambako amekutana na watu mbali mbali wakiwemo wakimbizi wa Syria waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa leo imesema amejadili nao hali ya sasa na mahitaji ya kibinadamu na maendeleo kwenye eneo hilo.

Huku kukiwa na matarajio makubwa kutoka mkutano wa kimataifa wa hali ya kibinadamu kuhusu Syria utakaofanyika Londom, mratibu huyo amesisitiza umuhimu wa Lebanon kuwa na utulivu wa kijamii sambamba na kuwa na uwezo wa kifedha ili kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi.

Amesema jamii ya kimataifa ina wajibu wa pamoja wa kuimarisha utulivu huo sambamba na ule wa kiusalama wakati harakati za kushughulikia athari za mzozo wa Syria zikiendelea.

Mwaka jana serikali ya Lebanon na wadau wa kimataifa waliomba dola Bilioni 2.4 kwa ajili ya kuhimili athari za mzozo wa Syria kwa mwaka huu wa 2016 ambapo mkutano wa London unalenga kuwa chachu ya kukidhi mahitaji hayo na athari za janga la Syria kwa nchi jirani.

Photo Credit
Picha: UNHCR/L. Addario