Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW58 wamulikwa
Mkutano wa 58 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, umeanza mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York.
Mkutano wa 58 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, umeanza mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York.
Vuguvugu la ustawi wa wanawake likiwa linaendela kwa mikutano mbalimbali hapa mjini New York inayoangazia hali ya kundi hilo, nchini Uganda katika kambi mojawapo ya wakimbizi wanawake wameshiriki katika mbio za baiskeli, kulikoni?
Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani unaendelea mjini New York na kando kunafanyika vikao mbali mbali kutathmini mwelekeo wa kundi hilo katika nyanja za kijamii, kisiasa, na kiuchumi.
Mwaka umeanza na mkutano mwingine wa kutathmini hali ya wanawake duniani umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Katika makala hii tunamulika maadhimisho ya siku ya wanawake tujiunge na Anthony Joseph wa radio washirika Wapo Radion FM ya Tanzania na kisha John Kibego wa radio washirika Spice FM huko Uganda.
Tarehe Nane Machi kila mwaka ni siku ya wanawake duniani! Ujumbe wa mwaka huu ni Usawa kwa wanawake Maendeleo kwa Wote!
Kuwapatia wanawake fursa katika nyanja zote ni muhimu kwa maendeleo ya kaya zao na hata taifa kwa ujumla.
Harakati za kukomboa wanawake zianze na wanawake wenyewe kwa kuweka ushirikiano zaidi badala ya kuhujumiana, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dkt. Albina Chuwa alipoulizwa na Idhaa hii kuhusu ujumbe wa siku hii wa Usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote!
Dunia ikiwa inaelekea kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Umoja wa Mataifa uko mstari wa mbele kuwawezesha wanawake katika maeneo mbalimbali ikiwamo afya ya uzazi, mazingira na hata kuwajengea uwezo wa kujiamini.
Ikiwa tunaelekea siku chache kabla ya siku ya wanawake duniani kilimo ni kiungo muhimu katika kuchagiza maendeleo na kuhakikisha uhakika wa chakula.