Kazi niliyotumwa Somalia nimeimaliza kwa wakati na kwa amani-Balozi Mahiga
Baada ya miaka mitatu ya kuhudumu kama Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema jukumu hilo lilikuwa ni kubwa na changamoto nyingi. Lakini alisonga mbele hadi kuwezesha kuundwa kwa serikali, bunge na katiba nchini humo.