Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 JULAI 2024

29 JULAI 2024

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akiangazia shambulio huko Sudan, kilimo biashara nchini Kenya. Makala inakupeleka Sudan Kusini harakati za mkimbizi aliyefurushwa mara mbili na sasa amerejea nyumbani na mashinani ni huko Paris Ufaransa kunakofanyika michezo ya olimpiki ya majira ya joto.

  1. Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidi
  2. Jitihada za kujikomboa na janga la njaa bado zinaendela nchini Kenya, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia kituo cha huduma kwa wakulima likiwapa wakulima elimu ya namna sahihi ya kuongeza uzalishaji licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo na hasa kwa kukumbatia kilimo biashara.
  3. Makala: Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR anakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia mkimbizi aliyelazimika kurejea nyumbani baada ya vita kuzuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka jana wa 2023.
  4. Mashinani: Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) Sima Bahous, akitoa kauli yake kuhusu kuwatambua na kuwapa fursa sawa wanariadha wa kike. Karibu!
Pakua

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'