Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP: Sera rafiki zinawainua kiuchumi wakimbizi nchini Uganda

WFP: Sera rafiki zinawainua kiuchumi wakimbizi nchini Uganda

Pakua

Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe.

Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.

“Niliondoka DR Congo sababu ya vita. Ninapokea Msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP lakini ukweli ni kuwa chakula hicho hakitoshi ndio maana nikahamia kwenye kilimo.”

Wakimbizi milioni 1.6 wanapatiwa hifadhi nchini Uganda, idadi hii ni mara nne zaidi ya idadi ilivyokuwa muongo mmoja uliopita. Wakimbizi wanapatiwa fursa ya kumiliki ardhi na kuyafikia masoko na hii inawapa fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe

“Nilikuwa mkulima nilipokuwa nchini kwangu na hapa niliungana na wananchi wa hapa pamoja na wakimbiziwengine na tukaanza kilimo cha mbogamboga. Tunashirikiana na wazawa na sote tunafundishana, tunalima nyanya, kabichi, maharage na matikiti maji. Mwezi uliopita niluza mazao yang una kupata dola 140, nilitumia fedha hizo kununua chakula na kukodisha ardhi zaidi ya kilimo.”

WFP inafanya kazi na wakimbizi na jamii zinazowakaribisha kujenga jamii zenye ustahimilivu.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'33"
Photo Credit
WFP/Marc Hofer