Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 JUNI 2024

20 JUNI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Japan kufuatilia harakati za kusongesha teknolojia rafiki na nafuu ili dunia iwe mahali salama kwa miti na binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo, na uchambuzi wa methali.

  1. Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi, Umoja wa Mataifa umeitumia siku hii kutoa wito wa mshikamano na wakimbizi kote duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema, "wanapopewa fursa, wakimbizi hutoa mchango mkubwa kwa jamii zinazowahifadhi."
  2. Mashambulizi ya Israel kwa kutumia mabomu kutoka angani, nchi kavu na baharini yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo zaidi vya raia, kuhama makazi yao, na uharibifu wa nyumba na miundombinu mingine ya raia, imeeleza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA.
  3. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limeipongeza Chad kwa kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa malale. Chad ni nchi ya kwanza kwa mwaka huu kutambuliwa kwa kutokomeza ugonjwa huo ulio katika kundi la magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs) na inakuwa nchi ya 51 kufikia lengo kama hilo ulimwenguni. Ugonjwa huu husambaa kutokana na binadamu kung’atwa na mdudu Mbung’o mwenye maambukizi.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Sauti
9'59"