Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanawake wabunge duniani imeongezeka kidogo 2023: IPU

Wagombea wa nafasi za Bunge la chini huko Somalia wakishiriki kwenye jukwaa la kisiasa nchini Somalia. (Maktaba)
AMISOM/Fardosa Hussein
Wagombea wa nafasi za Bunge la chini huko Somalia wakishiriki kwenye jukwaa la kisiasa nchini Somalia. (Maktaba)

Idadi ya wanawake wabunge duniani imeongezeka kidogo 2023: IPU

Wanawake

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni zaidi ya muungano wa mabunge duniani IPU kuhusu idadi ya wanawake bungeni 2023, idadi ya wabunge ambao ni wanawake duniani kote imeongezeka hadi asilimia 26.9, kutokana na uchaguzi na uteuzi uliofanyika mwaka 2023.

IPU inasema hii inawakilisha ongezeko la asilimia 0.4 mwaka baada ya mwaka, kiwango sawa cha ukuaji kwa mwaka 2022. 

Hata hivyo, ukuaji huo ni wa polepole kuliko miaka iliyopita kwani chaguzi za 2021 na 2020 zilishuhudia ongezeko la asilimia 0.6 ya wabunge.

Ripoti ya IPU inasema masuala ya kijinsia yalitawala chaguzi nyingi huku kukiwa na upinzani dhidi ya haki za wanawake katika baadhi ya nchi. 

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa wanawake kadhaa mashuhuri wameacha siasa hivi karibuni, wakilaumu uchovu na vitisho.

Ripoti hiyo ya IPU inatokana na marekebisho yaliyofanywa na bunge katika mabunge 66 kwenye nchi 52 mwaka 2023. 

Wanawake walikuwa asilimia 27.6 ya wabunge katika mabunge hayo mapya yaliyochaguliwa au kuteuliwa, ikiwa ni ongezeko la jumla la asilimia 1.4 ikilinganishwa na kura za awali katika nchi hizo hizo.

Nyanja zilizopiga hatua 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya IPU kulikuwa na maendeleo makubwa katika baadhi ya maeneo, kwa mfano:

Katika bara la Amerika, wanawake walichangia asilimia 42.5 ya wabunge wote waliochaguliwa au kuteuliwa katika mabunge ambayo yalichaguliwa upya mwaka wa 2023, asilimia kubwa zaidi ya kikanda. 

Kwa hivyo kanda hiyo inashikilia nafasi yake ya muda mrefu kama eneo lenye uwakilishi wa juu zaidi wa wanawake duniani, kwa asilimia 35.1.

Ulimwengunikote , sehemu ya Maspika wanawake wa mabunge iliongezeka hadi asilimia 23.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1. 

Cambodia na Côte d'Ivoire zilichagua Maspika wanawake kwa mara ya kwanza.

Viwango vilivyoundwa vyema na kutekelezwa vinaendelea kuwa jambo muhimu katika kuongeza uwakilishi wa wanawake. 

Mabunge 43 ambayo yalikuwa na aina fulani ya viti maalum yalichagua wabunge wanawake asilimia 28.8 kwa wastani, dhidi ya asilimia 23.2 katika nchi ambazo hazina.

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara 

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara IPU inasema ilirekodi uboreshaji wa juu zaidi kati ya kanda zote na ongezeko la asilimia 3.9 katika chaguzi za mwaka 2023 ikilinganishwa na kura za awali katika nchi hizo hizo. 

Mafanikio makubwa zaidi yalikuwa nchini Benin, Eswatini na Sierra Leone, yakiwezeshwa na nafasi za upendeleo.

Rwanda inaendelea kuongoza katika orodha ya kimataifa ya IPU huku wanawake wakichukua asilimia 61.3 ya viti katika Baraza la Manaibu, ikifuatiwa na Cuba na Nicaragua zenye asilimia 55.7 na 53.9 mtawalia, huku Andorra, Mexico na Umoja wa Falme za Kiarabu zikiwa na usawa.

Masuala ya jinsia yanatawala katika baadhi ya chaguzi

Ripoti ya IPU inabainisha kuwa masuala ya kijinsia mara kwa mara yaliibuka kama mazungumzo muhimu wakati wa uchaguzi mwaka 2023, hasa haki za uzazi za wanawake katika nchi ambapo utoaji mimba unasalia kuwa suala la kutatanisha.

Katika uchaguzi wa Poland, suala hilo lilikuwa kuu baada ya uamuzi wa mahakama wa 2020, ulioungwa mkono na serikali wakati huo, ambao ulizuia vikali fursa za utoaji mimba. 

Uamuzi huo ulifuatiwa na maandamano makubwa kote nchini, yakiongozwa na wanawake na vijana. 

Ripoti hiyo inadokeza kuwa hii ni sababu mojawapo iliyopelekea chama tawala kupoteza madaraka.

Kwa upande mwingine, Javier Milei, ambaye aliahidi kura ya maoni kufuta sheria zinazoendelea zaidi za utoaji mimba ambazo ziliwekwa mwaka wa 2020, alichaguliwa kuwa Rais wa Argentina. Ripoti nyingi.