Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Mocha kinaweza kusababisha 'hali ya kutisha' Myanmar: UN

Picha ya setilaiti ya Kimbunga Mocha siku ya Ijumaa.
© NOAA/NASA
Picha ya setilaiti ya Kimbunga Mocha siku ya Ijumaa.

Kimbunga Mocha kinaweza kusababisha 'hali ya kutisha' Myanmar: UN

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada ya kibinadamu wako tayari kutoa msaada wa dharura kwa jamii zilizoathiriwa na Kimbunga Mocha, kilichopiga katika Jimbo la Rakhine, Myanmar, leo Jumapili.

Kimbunga kikali sana, Mocha kiilikatiza pwani kati ya Cox's Bazar huko Bangladesh na jiji la Kyaukpyu nchini Myanmar wakati wa mchana Mei 14 kikisukuma upepo unaokadiriwa kuwa na kasi ya karibu kilomita 250 kwa saa na kuifanya kuwa moja ya vimbunga vikali zaidi vilivyorekodiwa katika miaka kumi iliyopita kwenye ukanda huo.

Mvua kubwa, mawimbi ya dhoruba na upepo mkali vimerekodiwa katika maeneo yaliyoathiriwa siku nzima, na mafuriko katika nyanda tambarare za Rakhine, hasa ndani na karibu na mji mkuu wa jimbo, Sittwe. Maelfu ya watu wametumia siku nzima kujihifadhi katika vituo vya uokoaji na nyumba za jamaa ndani ya nchi, ambapo watasalia usiku wa leo hadi upepo utulie.

Kutokana na hali mbaya ya hewa katika mji wa Rakhine na kukatika kwa mawasiliano ya simu, bado haijawezekana kutathmini ukubwa wa maafa hayo, lakini ripoti za awali zinaonesha kuwa uharibifu huo ni mkubwa na mahitaji ya jamii ambazo tayari ziko hatarini, hasa watu waliokimbia makazi yao, itakuwa muhimu.

Takriban watu milioni 6 tayari wanahitaji msaada wa kibinadamu katika majimbo ya Rakhine, Chin, Magway na Sagaing, ambako athari za kimbunga hicho zinatarajiwa kushuhudiwa. Kwa pamoja, majimbo haya ya magharibi ni nyumbani kwa watu milioni 1.2 waliokimbia makazi yao. Wengi wao wanakimbia migogoro na kuishi katika maeneo ya wazi, bila makazi ya kutosha.

Mamia ya maelfu ya watu wanaoishi katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh pia wako katika hatari kubwa. Ramanathan Balakrishnan, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Misaada ya Kibinadamu nchini Myanmar, amesema athari za kimbunga katika eneo ambalo mahitaji ya kibinadamu tayari ni makubwa ni "hali ya kutisha". Maelfu ya watu walio katika mazingira magumu, "ambao uwezo wao wa kubadilika umeharibiwa na migogoro mfululizo", wanaweza kuathirika.