2 Disemba 2019

Utamaduni wa ubakaji unaenea sana. Hii huingiliana na jinsi tunavyofikiria, tunavyoongea, na mienendo yetu ulimwenguni. Ingawa muktadha unaweza kutofautiana, utamaduni wa ubakaji huwa na mizizi katika mfumo dume, nguvu, na udhibiti.

Utamaduni wa ubakaji ni mazingira ya kijamii ambayo huruhusu unyanyasaji wa kijinsia kuwa hali ya kawaida na ya haki, inayochochewa na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia unaoendelea na mitazamo juu ya jinsia na ujinsia. Kuutaja ndio hatua ya kwanza ya kubomoa utamaduni wa ubakaji.

Kila siku tunayo fursa ya kuchunguza tabia na imani zetu kwa upendeleo unaoruhusu utamaduni wa ubakaji kuendelea. Sote tunaweza kuchukua hatua kupinga utamaduni wa ubakaji kwa mitazamo tuliyo nayo kuhusu utambulisho wa jinsia na sera tunazounga mkono katika jamii zetu. Unaweza kuchangia mbinu 16

1. Anzisha utamaduni wa maridhiano

Ridhaa iliyotolewa kwa bure ni lazima, kila wakati. Badala ya kutarajia “hapana”, hakikisha ni “ndio” ya nguvu kutoka kwa wahusika wote. Kubali ridhaa ya shauku katika maisha yako na uizungumzie.

2. Ongea dhidi ya visababishi vikuu.

Utamaduni wa ubakaji unaruhusiwa kuendelea wakati tunapokubali maoni ya kiume ambayo yanaona vurugu na utawala kama "nguvu" na "kiume", wakati wanawake na wasichana hawathaminiwi.

Pia inadhibitiwa na lawama kwa waathiriwa, mtazamo ambao unaochochea kuwa mwathirika badala ya mhalifu hubeba jukumu la mshambulio.

Katika majadiliano ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia, kama mwathirika alikuwa mlevi au la, nguo, na ujinsia hauna maana. Badala yake, zingatia kwamba wanaume na wavulana lazima wapate nguvu kupitia vurugu na uhoji wazo la ngono kama haki.

3. Ainisho jipya la uanaume

Jiulize kwa ukamilifu ni nini maana ya uaname kwako na jinsi unavyoutumia katika maisha yako. Tafakari ya kibinafsi, mazungumzo ya jamii, na usemi wa kisanii ni baadhi tu ya zana zinazopatikana kwa wanaume na wavulana; na vile vile wanawake na wasichana; kuchunguza na kufafanua upya maana ya uanaume na kanuni za kike.

UN Women
Siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake

 

4. Acha kumlaumu muathirika

Kwa maana lugha imeingiliana sana na tamaduni, tunaweza kusahau kwamba maneno na misemo tunayotumia kila siku huunda ukweli wetu.

Imani za kuthibitisha ubakaji zimo katika lugha yetu: "Alikuwa amevaa kama kahaba. Alitaka kubakwa, "

Hata ni sehemu ya mashairi ya nyimbo,  "Najua unaitaka."

Imefanywa hali ya kawaida kwa kutazama wanawake kuwa vitu na sio watu, na kuwaita majina duni katika utamaduni wa kimaarufu na vyombo vya habari.

Una uwezo wa kuchagua kuachana na lugha na nyimbo zinazowalaumu waathirika, kutothamini wanawake na kutoa udhuru wa unyanyasaji wa kijinsia. Kile mwanamke amevaa, ni nini na kwa  kiasi gani alikunywa, na alikokuwa wakati fulani, sio sababu ya kumbaka.

5. Katu usivumilie.

Weka sera za kutokuwa na uvumilivu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na vurugu kule unakoishi, unakofanya kazi, na unakocheza. Viongozi lazima wawe wazi kabisa kuwa wamejitolea kutekeleza sera ya kutokuwa na uvumilivu na kwamba lazima zitumike kila siku.

Kama hatua ya kuanza, angalia ni nini unachoweza kufanya kumaliza unyanyasaji kazini.

6. Ongeza wigo wa  uelewa wako kuhusu utamaduni wa ubakaji.

Kati ya wakati na muktadha tofauti, utamaduni wa ubakaji una aina nyingi. Ni muhimu kutambua kuwa utamaduni wa ubakaji unazidi wazo la mwanaume kushambulia mwanamke anapotembea pekee yake usiku.

Kwa mfano, tamaduni ya ubakaji inajumuisha aina nyingi ya mazoea mabaya ambayo hukwapua  uhuru na haki za wanawake na wasichana, kama vile ndoa ya utotoni na ukeketaji wa kike.

Tambua sababu zinazosisitiza utamaduni wa ubakaji na fikra potofu zinazouzunguka.

Ijapokuwa hakuna anayeweza kupinga kwamba ubakaji sio sawa, kupitia maneno, kutenda na kutotenda, dhuluma na unyanyasaji wa kijinsia ni jambo la kawaida na lisilo na uzito, inayotupeleka kwenye mteremko wa utamaduni wa ubakaji.

UN Women
Siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake

 

7. Chukua hatua mtambuka

Tamaduni ya ubakaji inatuathiri sote, bila kujali kitambulisho cha kijinsia, ujinsia, hali ya uchumi, kabila, dini au umri. Kuizua mizizi kunamaanisha kuacha ufafanuzi wa kizuizi wa kijinsia na ujinsia ambao unapunguza haki ya mtu kujifafanua na kujielezea.

Mienendo fulani kama vile mwelekeo wa kijinsia, ulemavu au kabila, na mambo kadhaa, huzidisha hatari ya vurugu kwa wanawake. Wapenzi wa jinsia moja na wale waliobadili jinsia zao, au LGBTQI wanaweza kuwa kwenye hatari ya “ubakaji wa urekebishaji” ambapo mhalifu hulenga kulazimisha mwathirika kufuata tabia iliyokaririrwa ya kijinsia na ujinsia. Wakati wa janga la kibinadamu, ubaguzi unaoenea kwa wanawake na wasichana mara nyingi huzidisha ukatili wa kijinsia.

Gulzada Serzhan, ni mwanachama hai wa Feminita, mpango wa wanawake Kazakhstan ambao unalinda na kutetea haki za kundi la LGBTQI. Alipokuwa akifanya kazi kama meneja wa mradi wa teknolojia ya habari, mfanyakazi mwenza wa kiume alianza kumnyanyasa kingono kwenye safari za biashara. Alipomwambia alikuwa mwenzi wa jinsia moja, unyanyasaji ukazidi.

 “Aliamini anaweza kunisahihisha. Alisema kwamba ninahitaji mwanaume mwenye nguvu,” Serzhan anasema.

8. Pata ujumbe kuhusu historia ya utamaduni wa ubakaji.

Ubakaji umetumika kama silaha ya vita na ukandamizaji katika historia. Umetumika kuwadhalilisha wanawake na jamii zao na kwa usafishaji wa kabila na mauaji ya kimbari.

 

9. Wekeza kwa wanawake.

Fadhili mashirika yanayowawezesha wanawake, hukuza sauti zao, husaidia manusura, na hukuza kukubali wa vitambulisho vyote vya jinsia na ujinsia.

10. Wasikilize manusura

UN Women
Siku ya kimataifa ya kutokomeza unyanyasaji dhidi ya wanawake

 

Katika enzi za #MeToo, #TimesUp, #NiUnaMenos, #BalanceTonPorc, na harakati zingine za mtandao, manusura wa vurugu wanapaza sauti na kuzungumza zaidi kuliko hapo awali.

Usiseme, “Kwa nini hakuondoka?”

11. Usifurahie ubakaji.

Ubakaji sio jambo la kuchekesha. Utani wa ubakaji hutohalilisha unyanyasaji wa kijinsia, hivyo kuwa ngumu kwa waathiriwa kusema wakati idhini yao inakiukwa.

Utani unaohalalisha dhuluma ya kijinsia haikubaliki. Kashifu!

Sema: “Tunakusikia. Tunakuona. Tunakuamini.”.

12. Jihusishe.

Utamaduni wa ubakaji unaendelezwa na kutokuwepo au ukosefu wa utekelezaji wa sheria zinazoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake na sheria za kibaguzi ya umiliki wa mali, ndoa, talaka na utunzaji wa watoto.

 

13. Kukomesha kutojali

Kukomesha utamaduni wa ubakaji, wahalifu lazima wawajibike. Kwa kushtaki kesi za unyanyasaji wa kijinsia, vitendo hivi vinaangaliwa kama uhalifu na tunatuma ujumbe mkali wa kutovumilia.

14. Kuwa mtazamaji anayejihusisha.

Moja kati ya wanawake watatu ulimwenguni wananyanyaswa. Ukatili dhidi ya wanawake ni kawaida, jambo la kushangaza, na tunaweza kushuhudia tabia zisizo na ridhaa au za dhuluma. Kuingilia kama ishara ya mwangalizi inamwashiria mhalifu kwamba tabia yake haikubaliki na inaweza kumsaidia mtu awe salama.

Kwanza, tathmini hali hiyo ili kuamua ni aina gani ya msaada, ikiwa wapo, unahitajika. Unaweza kumsaidia anaydhulumiwa kwa kuwajulia hali na kuuliza iwapo wanahitaji msaada, au kwa kurekodi tukio hilo, kuunda vitisho ili kutatiza hali hiyo, au kutoa taarifa fupi na wazi moja kwa moja kwa mhalifu kama vile, “Sifurahii unachofanya”.

Pata ujumbe jinsi unavyoweza kuwa mtazamaji mhusika, na uchukue mafunzo ya uingiliaji ambao unapangwa na chuo kikuu, manispaa, au mashirika yasiyo ya kiserekali za mitaa.

UN Women
Siku ya kimataifaya kutokomeza unyanyasaji dhidi ya wanawake

15. Elimisha kizazi kijacho.

Ikwe jukumu letu kuhamasisha wanawake wanaotetea haki za wanawake wa siku zijazo. Pinga mitindo iliyokaririwa ya kijinsia na maoni ya vurugu ambayo watoto hupatana nayo kwenye vyombo vya habari, barabarani, na shuleni. Watoto wako wajue kwamba familia yako ni nafasi salama kwao kujielezea walivyo. Sisitiza uamuzi wao na uwafundishe umuhimu wa ridhaa katika umri mdogo.

16. Anzisha au jiunge katika mazungumzo.

Zungumza na familia na marafiki kuhusu jinsi mnavyoweza kufanya kazi pamoja kumaliza utamaduni wa ubakaji katika jamii zenu.

Ikiwa ni kuanzisha kilabu cha mazungumzo ambacho kinafunua maana ya uanaume, kufadhili shirika la haki za wanawake, au kujiunga na vikosi vya kupinga maamuzi na sera zinazothibitisha ubakaji, itatuchukua sote kusimama pamoja dhidi ya tamaduni za ubakaji.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud