Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Katibu Mkuu wa UN António Guterres alipotembea shule iliyoathiriwa na kimbunga Idai kwenye kitongoji cha Munhava, mjini Beira nchini Msumbiji. (25 Juni 2019)

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: harakati isiyoweza kukomeshwa

UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa UN António Guterres alipotembea shule iliyoathiriwa na kimbunga Idai kwenye kitongoji cha Munhava, mjini Beira nchini Msumbiji. (25 Juni 2019)

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: harakati isiyoweza kukomeshwa

Tabianchi na mazingira

Baada ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu hatua kwa tabianchi uliotanguliwa na harakati za vijana kutaka hatua, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Antonio Guterres aliweka tafakuri  yake kwenye tahariri iliyochapishwa na ubia wa vyombo vya  habari 170  wenye wasomaji zaidi ya mamilioni.

Mabadiliko ya tabianchi

Katika maoni  yake yaliyochapishwa kwenye gazeti siku ya Alhamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “Umoja wa Mataifa, wafanyabiashara na watu ulimwenguni kote wanatia bidii kupambana na mabadiliko ya tabianchi, lakini juhudi hizi hazitoshi. Wakati wa mkesha wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hatua za tabianchi mnamo Septemba mwaka huu wa 2019, mamilioni ya vijana walihamasika kote ulimwenguni na kuwaambia viongozi wa ulimwengu kwamba wanawavunja matumaini, na kwa kweli hamna uongo kwenye hilo. Matokeo ya mabadiliko ya tabianchi tayari ni ya kuogofya unapoona athari kwenye bahari, misitu, mifumo ya hali ya hewa, bayonuwai, uzalishaji wa chakula, maji, kazi na hatimaye kwa maisha, na inatarajiwa kuendelea kuzoroteka zaidi. Sayansi hiyo haiwezi kukanwa, tazama tu mazingira yako, tazama kwenye dirisha”.

Wafanyakazi wa kujitolea wa shirika la hilali nyekundu nchini Bangladesh wakisaidia watu kuhamia maeneo salama kufuatia mvua kubwa na mafuriko kwenye eneo la Bandarban (July 2019)
Bangladesh Red Crescent Society/Bandarban Unit
Wafanyakazi wa kujitolea wa shirika la hilali nyekundu nchini Bangladesh wakisaidia watu kuhamia maeneo salama kufuatia mvua kubwa na mafuriko kwenye eneo la Bandarban (July 2019)

Serikali, vijana, biashara, miji, wawekezaji na asasi za kiraia wameungana kuchukua hatua ambazo ulimwengu unahitaji.

Bwana Guterres pia anasisitiza kwamba madhara ya tabianchi yanajitokeza kiuhalisia, kuanzia California hadi Karibea, Afrika hadi nchi ya kaskazini mwa dunia na kwingine, na kwamba ni wale ambao hawachangii sana janga hili ambao wanateseka zaidi.

“Natarajia mkutano huu wa hatua za tabianchi ambao viongozi wengi kutoka nchi nyingi walihudhuria utakuwa mwanzo wa mwelekeo ambao tutalazimika kuchukua ikiwa tunataka kufikia makubaliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris ifikapo mwaka wa 2020”, asema Bwana Guterres.

Zaidi ya nchi 70  zimeahidi kuondoa uzalishaji wa hewa ya ukaa  ifikapo mwaka wa 2050, ingawa nchi zinazozalisha kwa kiasi kikubwa bado hawajatoa ahadi. Zaidi ya miji 100 imejitolea, ikiwemo miji mikubwa zaidi ulimwenguni.

Greta Thunberg (kati kati), mwanaharakti wa maswala ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Sweden akiungana na vijana wanaharakati katika maandamano ya kila Ijumaa kwa ajili ya kuchagiza hatua kwa mustakabali kwenye Makao Makuu ya UN Agosti 30.
UN Photo/Manuel Elías
Greta Thunberg (kati kati), mwanaharakti wa maswala ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Sweden akiungana na vijana wanaharakati katika maandamano ya kila Ijumaa kwa ajili ya kuchagiza hatua kwa mustakabali kwenye Makao Makuu ya UN Agosti 30.

Karibu nchi 70 zimetangaza nia yao ya kutekeleza mipango yao ya kitaifa inayotokana na Mkataba wa Paris ifikapo mwaka wa 2020.

Kundi la nchi za visiwa vidogo, SIDS, limehakikisha kwamba litafanikisha kuondoa matumizi ya hewa ya  ukaa kwa kutumia nishati endelevu ifikapo mwaka wa 2030.

Nchi nyingi kama vile Pakistan, Guatemala, Colombia, Nigeria, New Zealand hadi Barbados zimeahidi kupanda miti zaidi ya bilioni 11.

Zaidi ya viongozi 100 wa sekta binafsi na kundi la wamiliki wakubwa wa mali duniani wameapa kuharakisha mabadiliko ya kampuni zao na rasilimali yao kwenye uchumi unaojali mazingira huku kikundi cha wasimamizi wa mali inayowakilisha karibu nusu ya fedha za dunia zilizowekezwa wameahidi kuwashawishi viongozi wa ulimwengu kupandisha bei ya hewa ya ukaa na kuondoa ruzuku kwenye mafuta ya kisukuku na nishati ya makaa ya mawe duniani kote.

mwanafunzi akiangalia a darasa  mpya linalojengwa shuleni mwao Sakassou mji wa kati wa Côte d'Ivoire kwa kutumia matofali yatoakanyo na taka za plastiki.
UNICEF/Frank Dejongh
mwanafunzi akiangalia a darasa mpya linalojengwa shuleni mwao Sakassou mji wa kati wa Côte d'Ivoire kwa kutumia matofali yatoakanyo na taka za plastiki.

Theluthi moja ya sekta ya benki ulimwenguni imejipa sharti la kuoanisha harakati zao na malengo ya mkataba wa Paris na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Katibu Mkuu anaongeza kuwa mkutano huo pia umeonyesha jinsi ambavyo miji na sekta kama vile usafirishaji wa meli zinaweza kufikia lengo la upunguzaji mkubwa wa uzalishaji wa  hewa chafuzi huku hatua za kulinda misitu na kuhakikisha usambazaji wa maji pia zilisisitizwa.

“Hatua hizi zote ni muhimu lakini hazitoshi. Tangu mwanzoni, mkutano huu uliundwa kuarifu ulimwengu na kuharakisha hatua kwa kiwango pana. Pia imetumika kama jukwaa la ulimwengu la kusikiliza ukweli mkali na kuangazia njia viongozi wote pamoja na wasio na hamu. Nitaendelea kuwahimiza kutia bidii zaidi ili kupata suluhisho za kiuchumi kijani ulimwenguni kote. Sayari yetu inahitaji hatua kwa kiwango cha kimataifa. Walakini, hii haiwezi kuhitimishwa mara moja na bila ushiriki kamili wa wale waliochangia sana kwenye janga hili. Ikiwa tunataka kuzuia mwamba wa tabianchi, zaidi inahitajika kufanywa ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na asilimia 45 ifikapo mwaka wa 2030, kutokomeza kabisa uzalishaji huo ifikapo mwaka wa 2050 na kupunguza ongezeko la joto kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selisiasi hadi mwisho wa karne. Ni kwa njia hii tu tunahifadhi  mustakabali wa ulimwengu wetu”, amesema.

Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Katibu Mkuu amaliza kwa kutoa maoni yake kuwa nchi nyingi zinaonekana kupendelea makaa ya mawe licha ya suluhisho la nishati zisizochafua mazingira. “Tunahitaji kuzidisha bei ya hewa ya  ukaa, kuhakikisha kuwa hakutakuwa na viwanda vipya vya makaa ya mawe ifikapo 2020 na kutopoteza pesa ambazo walipa kodi wanapata kwa ugumu katika kufadhili sekta ya mafuta ya kisukuku, ambayo inaongeza tu idadi ya watu wanaoathirika na vimbunga, vimbunga na kueneza magonjwa ya kitropiki na kuzidisha migogoro. Nitahakikisha kwamba ahadi hizi zinafikiwa kutoka mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika Desemba mwaka wa 2019 huko Santiago, Chile na Umoja wa Mataifa umeungana kusaidia utekelezaji wa mipango hii”.

Mabadiliko ya tabianchi ni suala kuu la wakati wetu na kuwa sayansi inaonyesha kwamba ikiwa hatutapata suluhisho, tutakabiliwa na ongezeko la joto kwa kipimo cha nyuzijoto 3 katika kipimo cha selisiasi ifikapo mwisho wa karne.

 “Sitakuwa hapa, lakini wajukuu wangu watakuwepo. Ninakataa kufumbia macho uharibifu wa makazi yetu pekee. Vijana, Umoja wa Mataifa na idadi inayoongezeka ya viongozi wa kibiashara, kifedha, serikali na mashirika ya kiraia, wengi wetu tunajihamasisha na kuchukua hatua. Walakini, tunahitaji wengi zaidi kufanikiwa katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi”.