Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 70 ya Tume ya sheria ya UN yaleta nuru

Rungu atumialo jaji mahakamani. (Picha:tovuti-ICTR )

Miaka 70 ya Tume ya sheria ya UN yaleta nuru

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Tume ya sheria ya Umoja wa Mataifa mwaka huu inatimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo imeelezwa kuwa uwepo wake umekuwa na mafanikio makubwa. 

Chris Maina Peter kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa wajumbe wa tume hiyo wanaokutana jijini New  York, Marekani amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii akisema kuwa…

Profesa Peter ambaye ni mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania akafafanua sheria hiyo inayozungumzia.

Kikao cha tume hii ambacho kwa kawaida hufanyika Geneva, Uswisi, kitaendelea hapa New York, hadi tarehe mosi mwezi ujao na baadaye kitaendelea huko Geneva kuanzia tarehe pili julai hadi 10 Agosti mwaka huu.